UTOAJI WA RUZUKU NDOGO KWA VIONGOZI WA SERIKALI NA MASHIRIKA YANAYOONGOZWA NA VIJANA.

Taasisi ya #DoorofHopetz pamoja na kazi kubwa tunazofanya za Kuhamasisha na kukuza uelewa kwa wananchi kuhusu masuala mbalimbali, Kujengea uwezo watendaji na kuimarisha mifumo ya utoleaji uhuduma za Jamii, kutoa mafunzo mbalimbali, pamoja na kufanya Utetezi wa uboreshaji wa sera, sheria, kanunu na miongozi mbalimbali, pia tunasaidia utoaji wa ruzuku ndogo kuwezesha watendaji na Viongozi wa Serikali za mitaa kutatua kero mbalimbali za makundi ya kijamii zinazoibuliwa na wananchi hususani Vijana na Wanawake.
Mwaka huu 2024 kwa mara nyingine tumefanikiwa kutoa ruzuku kwa mashirika na Ofisi za Vijiji, Kata na Halmashauri ili waweze kuimarisha mifumo ya utendaji na kutatua migogoro inayoibuka kwenye maeneo yao inayohusu Vijana, Watoto na Wanawake.
Ruzuku imetolewa kwenye Vijiji 24 vinavyopatikana kwenye Wilaya za Masasi, Tandahimba na Mtwara
Ruzuku imetolewa kwenye Kata 6 zinazopatikana kwenye wilaya za Masasi, Tandahimba na Mtwara
Ruzuku imetolewa kwa Mashirika 20 yanayoongozwa na Vijana kwenye Wilaya za Tandahimba, Masasi na Mtwara.
Ruzuku imetolewa kwenye Halmashauri za Masasi Tc, Mtwara DC na Tandahimba DC.Huu ni mwendelezo wa utoaji ruzuku tokea mwaka 2023 na ruzuku nyingine zilizotolea mwaka 2020.






