Mwanamke na Uongozi
Baada ya kutekeleza mbalimbali zinazolenga kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye Uongozi na kushika nafasi hizo kwenye ngazi mbalimbali za maamuzi, tumefanya tathmini wakati tukielekea kwenye uchaguzi wa serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu na kubaini mambo yafuatayo yanayohitaji ushiriki wa wadau mbalimbali.
1. Wanawake wamejiandaa kugombea lakini hofu ni gharama kubwa za uchaguzi kuanzi kuchukua fomu, gharama za usafiri, vipaza sauti na viburudishi wakati za zoezi la kampeni.
2. Wanawake wamejiandaa, wamejengewa uwezo na wana hari ya kushiriki kuwania nafasi ya uongozi, lakini wanakosa wasaidizi au wenza wao wenye uelewa huohuo ili kuwapigania wakati wa purukushani na hata kulinda kura zao au kukabiliana na hujuma mbalimbali Kipindi chaguzi za ndani ya vyama na kutangaza matokeo.
3. Wanawake wamejiandaa vema kugombea nafasi mbalimbali lakini baadhi ya wananchi wanaume kwa wanawake hawana imani nao, na tayari mira, desturi na imani ni vikwazo kwa baadhi ya maeneo kwenye kuamini uwezo wa wanawake na Wasichana. Na hivyo wanawake kuomba elimu na mikutano ya wazi ifanyike kuongeza elimu kwa jamii na hasa kipindi hiki.
4. Pamoja na kwamba kati hajatoa uhuru wa mgombea binafsi, wanawake wamejiunga na vyama mbalimbali ili viweze kuwapa dhamana ya kuingia kwenye kinyanganyiro cha Uongozi, changamoto inayotajwa na wanawake hawa ni urasimu, ukandamizaji, na baadhi ya Viongozi wa vyama kuwa na watu wao mapema. Hii inakatisha tamaa akina mama. Wanashauri Viongozi wa vyama mbalimbali wakutanishwe na kuelimishwa juu ya umuhimu kuzingatia makundi yote na kuwa na Uongozi jumuishi.
Kama Mwanaume, Mwanamke, Kijana wa Kike na Kiume ni nini ushauri wako ili tuweze kuwapata Viongozi wanawake kwenye nafasi mbalimbali ili waongoze na wanaume kwa pamoja?