Mijadala kwenye Majukwaa ya Vijana Halmashauri ya Nanyamba kata ya Kitaya, kwenye Vijiji vya Mayembe na Mchanje
Tunaendelea na uendeshaji na usimamizi wa mijadala kwenye majukwaa ya Vijana yanayohamasishwa na Vijana waleta mabadiliko na Viongozi wa serikali ngazi ya Kata na Vijiji.Majukwaa haya ni muhimu kwani yanatoa fursa kwa vijana kuweka wazi changamoto zao, changamoto za vijiji vyao na fursa zilizopo zinazopaswa kutumika kwa manufaa ya vijana na wananchi.
Masuala ya Ushiriki, utawala bora, uwazi wa mapato na miradi ya maendeleo, amani, usalama, rushwa, ukatili, uchakavu wa miundombinu na uhaba wa huduma za kijamii kama miundombinu ya elimu, afya, maji na barabara vimebainishwa.Maafisa wetu wanapata nafasi ya kushiriki, kutoa maoni, ushauri na kubeba masuala mengine yanayohitaji zaidi uchechemzi ngazi ya Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa.
Tunahakikisha masuala ya vijana na milalamiko yako yenye tija yanasikika, yanapewa kipaumbele, yanashughulikiwa na kupewa majibu stahiki kutoka kwenye mamlaka za umma na binafsi.