THRDC Meeting

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umetangaza na kutambulisha rasmi kamati ya Kitaifa ya uhamasishaji na ukusanyaji wa rasilimali za ndani zitakazo saidia shughuli za Utetezi wa haki za Binadamu.
Kamati hii inaundwa na Wakurugenzi 26 wa Mashirika yanayofanya kazi ya kutetea haki za Binadamu kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa #DoorofHopetz Bw. Clemence Mwombeki ni miongoni mwa Wakurugenzi wanaounda Kamati hiyo.Kwa sasa takribani 90% ya shughuli za utetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania unategemea ufadhili wa wadau wa kimataifa na mashirika ya Kimataifa, huku 10% pekee ikitokana na michango ya wadau wa ndani ya nchi na usaidizi wa Makampuni.









