KIKAO CHA MREJESHO WA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KIJANA KWANZA – MTWARA
Taasisi ya #DoorofHopetz tumekutana na Sekretarieti ya Mkoa wa Mtwara ikiongozwa na Katibu tawala wa Mkoa wa Mtwara.
Tumefanya majadiliano ya kimkakati tukiangazia kazi kutwa tunazofanya kwa kushirikiana na serikali ya Mkoa wa Mtwara kwenye halmashauri za Mtwara Mikindani, Mtwara Vijijini, Masasi na Tandahimba.
Tumejadiliana kwa kina maeneo na sekta zenye uhitaji wa jitihadi za wadau wa Maendeleo kama #DoorofHopetz na namna ya kuunganisha nguvu na wadau wengine.
Maeneo yaliyobainishwa kama afua zinazohitajika zaidi ni pamoja na uimarishaji wa uchumi kwa Vijana na Wanawake, afua zinazoongeza ujuzi na ajira kwa vijana, masuala ya utawala bora na ushiriki jumuishi kwa makundi ya kijamii, pamoja na afua zinazolenga kuondoa ukatili kwa wanawake, watoto wa kiume na kike.
Pamoja na #DoorofHopetz, tumeambatana na wadau wetu kutoka IRC (Regional and Country Program) pamoja na washirika wetu wa karibu kutoka MSOAPO, nia ni kuongeza nguvu na kutoa huduma kwa wigo mpana.