Event1
Leo 15/7/2020 Door of Hope tumewakutanisha Timu ya Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (SAM team members) na Mamlaka ya Maji ya Mkoa wa MTWARA (Mtwara Urban Water and Sanitation Authority – MTUWASA). Mwaka 2019 timu ya SAM ilifanya kikao na MTUWASA na kutembelea miradi na mifumo ya usambazaji wa maji sambamba na kupokea changamoto za Mamlaka. Kikao cha leo ni kujadili kwa kina namna ushauri na maoni ya Timu kwenye ripoti ya Uwajibikaji zimefanyiwa kazi, pia kikao hiki kinatazama miradi iliyokabidhiwa RUWASA na baadae MTUWASA iliyofuatiliwa na Timu ya SAM mwaka 2019. Zaidi Door of Hope inaweka mazingira mazuri ya timu ya SAM Kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Mamlaka ya Maji. Kikao hiki kinafanyika kwenye ofisi za MTUWASA#MajiniUchumi#majiniustawi#majiniafya#sammtwara#SAM2020