Event2

Door of Hope Tanzania yawaleta pamoja waandishi wa habari wa Vyombo vyote kutoka Mikoa ya Lindi na Mtwara. Nia ni kuwapitisha na kuwafahamisha Programu za kipaumbele zinazotekelezwa na taasisi kwenye Mikoa hiyo. Pia kuwajengea uwezo kwenye eneo la Ufuatiliaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (Social Accountability Monitoring) Kuwaongezea uelewa mpana wa dhana ya Usawa wa Kijinsia, Ukatili wa Kijinsia na Rushwa ya Ngono maeneo ya kazi, Vyuoni na Shuleni. Mafunzo haya yamefanyika Mkoani Lindi, Sea View Hotel